Timu ya KCCA ya Uganda imekuwa timu nyingine iliyojihakikishia tiketi ya kusonga mbele katika robo fainali ya mashindano ya vilabu bingwa Afrika Mashariki na kati maarufu kama kombe la Kagame. KCCA imeichapa Atletico ya Burundi goli 1 kwa bila, goli lililotiwa wavuni na mshambuliaji Alan Omony kwa njia ya penalti katika dakika ya 32. Atletico ambao wana pointi tatu wamebakiwa na mechi moja tu mkononi dhidi ya Telecom ambayo itaamua nafasi ya tatu ya kusonga mbele. Katika mechi nyingine ya kundi hilo, timu ya APR ya Rwanda nayo imefuzu katika robo fainali kufuatia ushindi wake wa goli 1-0 dhidi ya timu dhaifu ya Telecom ya Djibuti, mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali. Goli la kwanza lilipachikwa katika dakika ya 37 ambalo limefungwa na mlinzi Emery Bayisenge.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |