• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Muaustralia Dutton ashinda medali ya kwanza ya dhahabu kwenye Olimpiki ya vijana ya Nanjing

    (GMT+08:00) 2014-08-18 14:23:26

    Mwanariadha kutoka Australia Brittany Dutton amechukua medali ya kwanza ya dhahabu katika muchezo ya pili ya Olimpiki ya Vijana ya Nanjing kwa kushinda mbio za triathlon jana asubuhi. Dutton kwa jumla ametumia dakiaka 59 na sekunde 56, ambapo katika uogeleaji alikuwa nafasi ya saba kwa kutumia dakika 10:21, katika kuendesha baskeli km 20 alikuwa wa kwanza kwa kutumia dakika 31 na amemalizia mbio za km 5 pia akiwa wa kwanza kwa kutumia dakika 17:25. Nafasi ya pili katika mbio hizo ilichukuliwa na Mmarekani Stephanie Jenks ambaye amepata medali ya fedha kwa kutumia muda wa saa 1 na nukta 33, huku nafasi ya tatu ikienda nchini Ufaransa kwake Emilie Morier aliyetumia muda wa 1:00: 55 na kuondoka na shaba na nafasi ya nne ikaenda kwa Kristin Rawning kutoka Ujerumani. Awali mwanariadha kutoka Japan alikuwa akiongoza katika hatua ya uogeleaji, ambapo amemaliza akiwa ametumia dakika 10 na sekunde 5, hata hivyo alikuwa nusura azongwe na kamba wakati anatoka kwenye maji lakini aliweza kwenda kupanda baiskeli akiwa wa kwanza. Michuano hii inaendelea hadi Agosti 28, ambapo jumla ya michezo 28 inashindaniwa na wanariadha 3,700 wenye umri wa miaka kati ya 15 na 18 kutoka nchi mbalimbali duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako