Waziri wa michezo wa Nigeria Tammy Danagogo amesema mwenyekiti wa Chama Cha Soka nchini humo Aminu Maigari atarejea kazini kuanzia leo. Kurejea huko kunatokana na makubaliano yaliyohusisha pande zote zilizokuwa na mgogoro ili kuhakikisha kwamba tatizo linaondolewa. Bodi ya NFA ilimsimamisha kazi Maigari kwa sababu za matumizi mabaya ya fedha na uongozi mbaya, na kutoka hapo ilimteua makamu wa kwanza wa mwenyekiti Mike Umeh kukaimu nafasi ya mwenyekiti. Hata hivyo Shirikisho la Soka Duninai FIFA, lilitaka lipewe maelezo ya kina na sababu zilizopelekea kusimamishwa kwa Maigari, ambapo bodi NFA ilijibu, lakini katika barua nyingine Fifa ilishauri kuwa Maigari aruhusiwe kuwa mwenyekiti kutokana na baraza la NFA litakalofanyika Agosti 26. Sasa waziri amesema mgogoro uliopo umemalizwa na wajumbe wa bodi wamekubali kufanyakazi na Maigari ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa wepesi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |