• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Van Gaal aanza kuionja joto ya jiwe

    (GMT+08:00) 2014-08-18 14:25:10

    Kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal alionja joto ya jiwe baada ya kucharazwa mabao 2-1 dhidi ya Swansea katika mechi yake ya kwanza ya ligi kuu ya Uingereza msimu huu. Licha ya kushabikiwa na maelfu ya mashabiki alipoingia uwanjani Old Trafford, Manchester united iliambulia kichapo cha kwanza tangu mwaka wa 1972. Kocha huyo aliyeiongoza Uholanzi kumaliza katika nafasi ya tatu huko Brazil katika Kombe la Dunia, alijaribu mbinu zote lakini hazikufua dafu baada ya Swansea kuyatumia vizuri makosa ya safu ya Ulinzi ya United katika dakika ya 28 kipindi cha kwanza. Bao hilo liliwaamsha Swansea usingizini na mechi hiyo ikawa tena na msisimko mkubwa baada ya mashambulizi ya United yaliposhindwa kuzaa matunda huku Swansea nayo ikijaribu kufanya mashambulizi dhidi ya united. Gylfi Sigurdsson alivunja matumaini ya mashabiki wa united alipofunga bao la ushindi katika dakika ya 72 na kuihakikishia Swansea ushindi wake wa kwanza. Wakati huohuo Liverpool nao wamepata ushindi wa mabao 2-1 na kujizolea pointi tatu muhimu dhidi ya Southampton katika mechi yao ya kwanza ya ligi kuu msimu huu bila ya mshambuliaji wao wa kutegemewa Suarez. Nayo Arsenal ikionesha cheche zake katika msimu huu kwa kuilaza Crystal kwa mabao 2-1, huku Leicester ikatoka sare ya 2-2 na Everton. QPR kwa upande wake iliambulia kichapo cha 0-1 dhidi ya Hull, Stoke nayo ikipoteza kwa matokeo sawa na hayo dhidi ya Aston Villa. Awali West Brom ilitoka sare ya 2-2 na Sunderland, nayo West Ham ikalimwa 0-1 na Tottenham.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako