Akiwa mwanagimnastiki wa kwanza kutoka visiwa vya Cayman kushindana kimataifa, Morgan Lloyd ameweka historia katika kamati ya Olimpiki ya nchi yake NOC. Lloyd alifuzu kushiriki michezo hii kupitia michezo ya mabingwa ya Pan American iliyofanyika nchini Brazil mwezi Machi. Katika mashindano hayo pia aliweka rikodi ya kitaifa na yake binafsi kwa kupata pointi 39.334. mchezaji huyo wa kike mwenye miaka 15 aliivunja rikodi hiyo jana kwa kupata pointi 41.250. Lloyd amesema amefurahi kuona maandalizi yake ya kiakili yamepata mafanikio makubwa huko Nanjing. Wakati huohuo Jiang Huihua ameshinda medali ya kwanza ya dhahabu kwa upande wa wanariadha wa China katika michezo hiyo ya Olimpiki ya Vijana baada ya kubeba uzito wa kilo 48 kwa upande wa wanawake. Jiang alifanikiwa kubeba uzito wa Kg 88, 105kg na kumalizia na kg 193, uzito ambao ni mara nne ya uzito wake wa mwili ambao ni kg 47.3. kwa upande wa uogeleaji bingwa wa dunia na Olimpiki Ruta Meilutyte wa Lithuania ameshinda baada ya kuogelea kwa mtindo wa Breaststroke mita 50. Msichana huyo alitawala mchezo huo na kufanikiwa kugusa ukuta akiwa ametumia sekunde 30.14 ambayo ilikuwa ni kasi kubwa kwa mara tatu mwaka huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |