Mshambuliaji Daniel Sturridge amesema Liverpool ina nguvu kubwa msimu huu, licha ya kuanza bila ya mfungaji bora wa mwaka jana Luis Suarez. Alipoulizwa kama timu hiyo bado ni bora kufuatia kuondoka kwa Suarez alisema kutokana na wachezaji wapya timu ni nzuri sana, na kwamba ingawa Suarez ni mchezaji mzuri lakini wameamua kusonga mbele. Mshambuliaji wa Uruguay Suarez ambaye amehamia Barcelona kwa ada ya uhamisho pauni milioni 75, amefunga mara 31 katika mechi 33 alizocheza ambapo Reds walichukua nafasi ya pili msimu uliopita. Liverpool imewasaini wachezaji wanane tangu kumalizika kwa msimu uliopita kwa gharama ya pauni milioni 101. Watatu kati yao Javier Manquillo, Dejan Lovren na Rickie Lambert walicheza kwenye mechi ya juzi dhidi ya Southampton
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |