• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SADC haitaweka marufuku ya kusafiri kutokana na homa ya Ebola

    (GMT+08:00) 2014-08-19 10:24:13

    Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC imesema haitaweka marufuku ya usafiri kwa nchi za Afrika Magharibi zilizokumbwa na homa ya Ebola. Katibu Mtendaji wa SADC Bw Stergomena Tax amesema wakati nchi mbalimbali duniani zinaendelea kupambana na Ebola, mipaka ya nchi jirani inafungwa na mashirika ya ndege yanasimamisha safari zao kwenye nchi zilizoathiriwa, Jumuiya ya SADC haitafanya hivyo.

    Wakati huo huo nchi mbalimbali zinaendelea na hatua za kupambana na homa ya Ebola. Mjini Addis Ababa Umoja wa Afrika na mashirika ya misaada ya kimataifa yameitisha mkutano kuangalia njia ya kushirikiana kupambana na ugonjwa huo. Cameroon imefunga mpaka wake na Nigeria ili kuzuia virusi vya ugonjwa huo kuingia Cameroon. Na Rais Alpha Conde wa Guinea ametangaza hali ya hatari kiafya kutokana na homa ya Ebola.

    Kundi lingine la madaktari wa China wa kupambana na magonjwa ya mlipuko wamewasili nchini Guinea kusaidia juhudi la kupambana na ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako