• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa IOC ataka kutumia michezo ya YOG kuboresha michezo ijayo

    (GMT+08:00) 2014-08-20 10:58:18

    Kamati ya Olimpiki ya kimataifa inataka kutumia michezo inayoendelea ya Olimpiki ya Vijana ya Nanjing kama jaribio la kuweza kuboresha zaidi uendeshaji wa michezo hiyo pamoja na njia za kuchagua nchi waandaaji. Rais wa kamati hiyo Thomas Bach amesema kutokana na kiwango na gharama za mashindano makubwa ya michezo, kuandaa Olimpiki imekuwa kazi yenye changamoto kubwa hususan kwa nchi zinazoendelea, ambazo zimekwamisha kuenea moyo wa Olimpiki. IOC inampango wa kufanya mageuzi kwenye mchakato wa kutafuta nchi ya kuandaa michezo hiyo na kubadilika katika michezo na kiwango cha michezo. Hadi sasa Bach ambaye ni mshindi wa medali ya dahahbu katika mchezo wa fensi mwaka 1976 huko Montreal ameridhishwa na kazi ya kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya Nanjing, ya kuweza kuwasilisha michezo katika njia imara. Bado masuala ya ugumu kwa nchi zinazotarajia kuandaa mashindano makubwa umeanza kutokeza hususan baada ya Vietnam kutangaza mwezi Aprili kuwa inajitoa kuandaa michezo ya Asia ya mwaka 2019 kutokana na ukosefu wa fedha na uungaji mkono wa nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako