• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fan wa China atia nia ya kuwa bingwa wa Olimpiki na Olimpiki ya Vijana

    (GMT+08:00) 2014-08-20 10:58:53

    Kwa wanariadha wengi wanaoshiriki michezo ya pili ya Olimpiki ya Vijana ya Nnajing, ni jaribio la kwanza kuona inavyokuwa unaposhindana kimataifa. Lakini kwa nyota wa mpira wa meza wa China Fan Zhendong Olimpiki ya Vijana inaweza kuwa ni hatua ya kuelekea kufanya vizuri zaidi. Hivi sasa Fan ambaye yupo katika nafasi ya tatu duniani, tayari ameshaweka historia baada ya kuwa bingwa mdogo kabisa wa ITTF duniani akiwa na miaka 16. Fan alishinda mechi zake nne za mwanzo mjini Nanjing kwa ushindi wa seti 3-1, 3-0, 4-1 na 3-0. Licha ya ushindi huo, haikuwa safari nyepesi. Baada ya kushindwa seti ya kwanza katika mechi ya kwanza dhidi ya Brian Afanador wa Puerto Rico, alirudi kwa nguvu zote na kushinda mechi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako