Max Verstappen mwenye miaka 16 amesisitiza kuwa ni hatari kuendesha baiskeli katika miji mikubwa kuliko kushindana kwenye mashindano ya gari ya Formula 1, baada ya kusainiwa kuendesha katika timu yaToro Rosso. Mholanzi huyo atakuwa dereva mdogo zaidi katika historia ya mashindano ya magari atakaposhindana mwakani. Verstappen ambaye mwezi ujao anafikisha miaka 17, hivi sasa anashindana kwenye formula 3. Verstappen ni mtoto wa dereva wa zamani wa formula 1 Jos ambaye sasa ana miaka 42, na ameshashindana mara 106 katika grand prix kwa timu kama Benetton na Tyrrell kati ya mwaka 1994 na 2003. Rikodi hiyo ya dereva mdogo kwa sasa inashikiliwa na muhispania Jaime Alguersuari, ambaye alianza kushindana akiwa na miaka 19 na siku 125 nchini Hungury, pia akiwa na timu ya Toro Rosso mwaka 2009. Alguersuari aliondoka Toro Rosso na F1 mwishoni mwa msimu wa mwaka 2011.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |