Baada ya usajili wa Ander Herrera na Luke Shaw, klabu ya Manchester United juzi ilikamisha usajili wa mchezaji mwingine. Marcos Rojo, beki kutoka Argentina aliyekuwa anasakata kabumbu kwenye klabu ya Sporting Lisbon amethibitishwa rasmi kujiunga na kikosi cha Louis Van gaal. Rojo ambaye alichaguliwa katika kikosi bora cha kombe la dunia, amejiunga na United kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 16 pamoja na Luis Nani kwenda Sporting kwa mkopo miaka saba baada ya winga huyo kujiunga na United akitokea Lisbon. Wiki iliyopita Rojo aligoma kufanya mazoezi na Sporting kufuatia kuchanganyikiwa kwa kutoruhusiwa kuondoka, ingawa baadaye aliomba radhi. Rojo amesema itakuwa ndoto kubwa kwake kuichezea United. Imefahamika kuwa hivi sasa Manchester United wanahamishia nguvu zao kwa Angel di Maria wa Real Madrid.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |