• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magwiji wa timu ya Real Madrid ya Hispania wawasili nchini Tanzania

    (GMT+08:00) 2014-08-21 10:34:49

    Kundi la kwanza la wachezaji nyota wa zamani kutoka kikosi cha Magwiji wa timu ya Real Madrid ya Hispania (Madrid Legends) linatarajia kutua nchini Tanzania leo, tayari kwa maandalizi ya ziara ya siku Tano ya timu hiyo ya maveterani waliowahi kuwika na kufanya makubwa katika timu ya Real Madrid. Mratibu wa ziara hiyo Evarist Hagira amesema kikosi cha magwiji hao kitakamilika kesho Agosti 22 kwa kundi lililobaki kutua nchini Tanzania, ambapo Jumamosi watavaana na kikosi cha wachezaji magwiji wa Tanzania (Tanzania All Stars). Hagira amesema kiujumla maandalizi yote ya ziara ya magwiji hao ambayo inajulikana kama utalii wa kimichezo huko nchini Tanzania yamekamilika. Hagira ametaja kundi la kwanza la baadhi ya wachezaji wanaotarajiwa kwenda ni pamoja na wakongwe Luis Figo, Michael Owen, Fabio Canavaro na Christian Kalembeu na kundi lingine ambalo litakuwa na wachezaji wengine na mashabiki wanaofikia 50 litatua siku moja kabla ya timu hiyo kuvaana na timu ya nyota wa zamani waliowahi kuwika na vilabu mbalimbali vya Tanzania kama kipa Mohamed Mwameja, beki Boniface Pawasa, Edibili Lunyamila na wengine wengi. Ziara yao itatoa funzo kwa vijana na itafungua fursa ya ushirikiano katika nyanja za kimichezo, kijamii na kiuchumi kwa kuwa watatembelea pia baadhi ya vivutio vya utalii nchini Tanzania

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako