• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wairaq watumia filamu kusimulia maisha ya watu waishio vitani

    (GMT+08:00) 2014-08-21 17:50:46

    Kwenye masikio ya wengi, jina Iraq linahusiana na vita, milipuko na vifo vinavyoelezwa katika vichwa vya habari. Lakini kwa wale wanaoishi nchini humo, nchi hiyo ni nyumbani kwao ambako wanaishi jamaa na marafiki zao, na watengeneza filamu nchini Iraq wanajitahidi kutumia ustadi wao kurekodi maisha yanayoendelea katika ardhi hiyo.

    Jengo la ghorofa mbili lililokuwa makazi ya aliyekuwa waziri wa fedha wa kwanza Iraq liko kando ya mto Tigris. Kituo cha filamu cha Iraq kiko ndani ya jengo hilo. Watengeneza filamu wa Iraq wanatumia kazi zao kuwaelezea watu walio nje ya Iraq hali iliyoendelea na inayoendelea nchini humo. Bw Yahya al-Allaq ni mmoja wa watengenezaji filamu wa kituo hicho.

    "watu walio nje ya Iraq wanaifahamu Iraq kupitia habari zinazotolewa na vyombo vya habari, kama vile milipuko, magaidi, na kundi la ISIS. Habari hizi sana sana zinajaa takwimu, lakini sisi tunataka kueleza ni nini kinachoendelea hapa. Watu wanavyoishi, wanavyowasiliana na wengine, wanavyokabiliwa na tishio la kifo, haya yote yasiyo rahisi ndiyo tunayotaka kueleza. "

    Bw Yahya al-Allaq aliwahi kusomea utengenezaji wa filamu nchini Marekani, na kupata shahada ya pili. Filamu zake nyingi alizitengeneza kutokana na matukio halisi yaliyotokea wakati wa vita kati ya Iraq na Iran, na wakati Iraq ikivamiwa na Kuwait na Marekani. Ametaja filamu anayotengeneza sasa inayohusu maisha ya watu wa Mosul, ambao baadhi yao wanaishi maeneo yaliyotekwa na kundi la ISIS.

    "Filamu hii inahusu kijana mmoja na mdogo wake. Watu wenye msimamo mkali waliingia nyumbani kwao kwa nguvu na kumwua mama yao. Vijana hawa wawili walinusurika mauaji haya na kukimbilia mahali salama. Njiani walikutana na watu wa aina mbalimbali."

    Bw Yahya al-Allaq anasema kupitia filamu hii, anataka kuwafahamisha watu kwamba, Wairaq bila kujali ni dini au kabila gani wanapitia uchungu wa aina moja. Anasema picha wanayotakiwa kupewa watu kuhusu Iraq haitakiwi kuhusu vita na vifo tu, nchi hiyo pia ina usanii wa kujivunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako