• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eto'o atolewa kwenye kikosi cha taifa cha Cameroon

    (GMT+08:00) 2014-08-25 10:16:47

    Cameroon imefanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, kwa kuwaacha wachezaji 13 ambao walicheza kombe la dunia akiwemo Samuel Eto'o. Kocha mzaliwa wa Ujerumani Volker Finke ambaye anaendelea kukinoa kikosi hicho licha kufanya vibaya nchini Brazil, ametangaza sura mpya za kikosi cha wachezaji 25 juzi kwa ajili ya mashindano yajayo ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika. Eto'o amekuwa hana timu tangu aachiwe na Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita, na hatua hiyo ya kutoshirikishwa haikushangaza sana, kwani hajacheza tangu kwenye mechi moja tu ya kombe la dunia dhidi ya Mexico. Kiungo Alex Song naye pia yupo nje akitumikia adhabu yake baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wa Croatia Mario Mandzukic wakati wa kombe la dunia, huku mshambuliaji Henri Bedimo akijeruhiwa mapema mwezi huu. Pia mchezaji mwingine aliyeachwa ni Benoit Assou Ekotto, ambaye alijaribu kumpiga mchezaji mwenziwe wa timu yake Benjamin Moukandjo walipocheza na Croatia na kushindwa kwa mabao 4-0.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako