• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchezaji kutoka Cameroon afariki nchini Algeria baada ya kupigwa na kitu na mashabiki

    (GMT+08:00) 2014-08-25 10:17:28

    Mchezaji mmoja wa soka raia wa Cameroon Albert Ebosse amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu kichwani mwake kilichorushwa na mashabiki mwishoni mwa mechi katika ligi ya Algeria. Mshambuliaji huyo wa JS Kabylie mwenye umri wa miaka 24, ambaye aliifunga timu yake bao la pekee katika mechi hiyo waliyoshindwa na USM Alger kwa 2-1, alipigwa na kitu wakati mashabiki walipoanza kurusha vitu wakati timu zilipokuwa zikienda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mechi kumalizika. Waziri wa mambo ya ndani nchini Algeria ameagiza kuanzishwa uchunguzi kuhusu mauaji hayo. Ebosse alikuwa ni mfungaji anayeongoza katika ligi ya Algeria katika msimu wa mwaka 2013/14, akiwa na jumla ya magoli 17. Hadi sasa haijajulikana Ebosse alipigwa na kitu gani, lakini gazeti moja nchini humo limesema mashabiki wa timu wenyeji, waliokasirika kwa timu yao kufungwa nyumbani, walikuwa wakirusha mawe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako