Bingwa wa mara tatu wa Olimpiki na dunia Usain Bolt ameshusha zaidi muda wake chini ya sekunde 10 kwa mara ya kwanza mwaka huu kwa kukimbia kwa sekunde 9.98 huko Poland, na kuweka rikodi isiyo rasmi ya dunia kwa mbio za mita 100. Hii ni mara ya pili kushindana msimu huu baada ya kupata jeraha la mguu. Amerejea kushindana tena kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola, na kuipatia medali ya dhahabu nchi yake katika mbio za kupokezana vijiti mita 100 mara 4. Mkimbiaji huyo anayeshikilia rikodi ya dunia atachuana tena siku ya Alhamis huko Zurich, ambapo atashindana na Britons Adam Gemili na James Dasaolu katika ligi ya Diamond nchini Uswizi.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |