Mkimbiaji wa China Liang Xiaojing ameshinda mbio za mita 100 katika michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Nanjing. Ling alikimbia kwa muda wa sekunde 11.65 na kuongoza baada ya mkimbiaji aliyekuwa akitegemewa kupata ushindi Nikola Swoboda kutoka Poland, kushindwa kuchukua ushindi kufuatia makosa aliyofanya katika sehemu ya kuanzia mbio. Msichana huyo atakuwa ni mchina wa kwanza kabisa kushinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 100 kwenye michezo ya Olimpiki. Wakati huohuo ikiwa zimesalia siku tatu kabla ya ufungaji wa michezo ya pili ya Olimpiki ya vijana ya Nanjing, rais wa kamati ya Olimpiki ya kimataifa Thomas Bach ameipongeza sana michezo hiyo akisema amefurahia alichokiona Nanjing. Amesema amevutiwa na mpangilio na maandalizi ya michezo hiyo. Kwa upande wa wanariadha mbalimbali nao wamesema pia wanafurahia michezo na kwamba wana wasiwasi kama nchi mwenyeji wa michezo inayofuata itaweza kufikia kiwango hicho.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |