• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Louis van Gaal asema ubingwa ni muujiza mkubwa kwa Manchester United

    (GMT+08:00) 2014-08-26 10:41:32

    Kocha Mkuu wa Manchester United, Louis van Gaal amesema itakuwa ni muujiza mkubwa kwa timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu. Mdachi huyo ameilinganisha United ya sasa na Bayern Munich ya mwaka 2009 wakati alipokuwa akiinoa timu hiyo iliyokuwa na kikosi kilichokuwa na kasoro nyingi. Hata hivyo, Van Gaal akamaliza ligi msimu huo kwa kunyakua Ubingwa wa Bundesliga, kitu ambacho haoni kama kitaweza kujirudia kwa sasa akiwa na United. Wasiwasi wa Van Gaal umeibuka baada ya wiki iliyopita kuchapwa na Swansea City nyumbani Old Trafford katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu England.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako