• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi ya Algeria yasimamishwa kufuatia kifo cha Ebosse

    (GMT+08:00) 2014-08-26 10:42:03

    Shirikisho la soka la Algeria limesimamisha ligi kuu ya soka nchini humo kufuatia kifo cha mchezaji kutoka Cameroon Albert Ebosse, ambaye alipigwa jiwe lililorushwa na mashabiki. Uamuzi huo umefikiwa baada ya shirikisho kukutana juzi Jumapili. Shirikisho hilo limeamua kufunga viwanja vyote nchini humo na kusimamisha mechi zote hadi pale mikakati mipya ya kudhibiti utovu wa nidhamu na kuhakikisha usalama wa wachezaji itakapotangazwa. Pia limeahidi kutoa dola laki moja kwa jamaa na familia ya Ebosse kiasi kinachoaminika kuwa sawa na mshahara wake iwapo angemaliza mkataba wake katika klabu hiyo ya JS Kabylie. Na kila mchezaji wa klabu hiyo atatoa mshahara wake wa mwezi mmoja kusaidia familia ya Ebosse. Awali Rais wa shirikisho la soka barani Afrika Issa Hayatou alionya kuwa Afrika haitatumika kama chimbuko la utovu wa nidhamu. Hayatou aliagiza hatua kali za kisheria kuchukuliwa ili kukabiliana na utovu wa nidhamu. Rais wa ligi kuu ya Algeria Mahfoud Kerbadj, alisema kuwa kifo chake ni msiba mkubwa kwa soka ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako