Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), limeiacha kinywa wazi Yanga kwa kutamka halina kanuni ya kuiadhibu kwa kosa lililofanywa na klabu hiyo zaidi ya vile ilivyoiondoa kwenye Kombe la Kagame. Yanga iliondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kupeleka kikosi cha vijana jambo ambalo liliikera Cecafa na ikuamua kuipa nafasi Azam FC. Cecafa imefafanua kwamba kama Yanga ingekwenda kwenye mashindano na kufanya utovu wa nidhamu wangekuwa na nguvu ya kuwashughulikia kikanuni lakini kwa kupeleka kikosi dhaifu adhabu ni kuwaondoa tu mashindanoni. Rais wa Cecafa, Leodegar Tenga ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, alisema hakuna kipengele kinachoweza kuwahukumu Yanga kwa kitendo cha kutotuma timu A.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |