Inadaiwa kuwa beki mpya wa Manchester United, Marcos Rojo anaweza kukumbana na kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kufanya kosa la kumpiga chupa jirani yake miaka minne iliyopita. Beki huyo ambaye alitua United wiki iliyopita kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 16 huenda akapandishwa mahakamani huko kwao Argentina. Inadaiwa kwamba Rojo (24), alimshambulia kwa chupa jirani yake, Juan Pablo Gomez katika tukio lililotokea mwaka 2010. Licha ya kwamba tukio hilo limetokea miaka minne iliyopita, waendesha mashtaka bado wanaangalia uwezekano wa Rojo kupandishwa kizimbani kwa mujibu wa Gazeti la The People. Ripoti hiyo ilibainisha kwamba mwendesha mashtaka, Marcelo Romero kwa sasa anasubiri kauli za wanasheria wa mchezaji huyo. Akikutwa na hatia, anaweza kufungwa miezi 12 jela.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |