Kocha Mkuu wa Liverpool, Brendan Rodgers amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo na kuwaambia wasiwe na shaka na Mario Balotelli anafahamu namna ya kumtuliza na atatulia. Kwanza Rodgers alisema hatamruhusu Balotelli aende kuishi Manchester, mahali ambapo alikuwa na matukio mengi ya ajabu wakati alipokuwa akikichezea kikosi cha Manchester City. Rodgers alisema atataka Balotelli aishi mitaa ya karibu na wachezaji wenzake wa Liverpool ili iwe rahisi kwake kumfuatilia nyendo zake. Kocha huyo anaamini ataweza kumtuliza na kumfanya Balotelli aache utukutu wake na kucheza mpira. Rodgers pia amesema Baloteli amepata nafasi ya mwisho baada ya kusainiwa na Liverpool kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 16 kwa mkataba wa miaka mitatu. Liverpool imeanza kumfanyisha mazoezi jana Jumanne na anaweza kuwamo kwenye kikosi kitakachomenyana na Tottenham Hotspur Jumapili wiki hii.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |