• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Everton yamsaini mshambuliaji nyota kutoka Cameroon Samuel Eto'o

    (GMT+08:00) 2014-08-28 10:21:37

    Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya FC Barcelona na Chelsea Samuel Eto'o amekamilisha usajili wa kujiunga na Klabu ya Everton pamoja na kwamba alikuwa akikaribia kujiunga na Liverpool. Everton imemsaini kwa mkataba wa miaka miwili ambapo nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon ameripotiwa kusononeshwa na uhamisho wake wa kwenda Liverpool kufeli wakati akiwa tayari alishafanya mpaka vipimo vya afya. Mshambuliaji huyo aliruhusiwa kuondoka Chelsea mwisho mwa msimu uliopita. Liverpool walionesha nia ya kumsajili lakini mchezaji huyo hakuhimili ushindani kutoka kwa Mario Balotelli. Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka huko Goodison, huenda mshambuliaji huyo akashiriki mechi ya kufungua msimu baina ya Everton na Chelsea siku ya Jumamosi. Everton tayari wamemsajili Romelu Lukaku kutoka Chelsea kwa gharama ya pauni milioni £28 mbali na kumsajili Christian Atsu kwa mkopo. Mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuwa mchezaji nyota barani Afrika kwa miaka minne aliifungia Anzhi Makhachkala mabao 12 katika mechi 35 alizoshiriki. Eto'o pia amewahi kuichezea mahasimu wakuu katika ligi kuu ya Uhispania Real Madrid na Barcelona. Alipokuwa Nou Camp, alitwaa ubingwa wa ligi ya Ulaya mara mbili katika mwaka 2006 na 2009. Eto'o alijiunga na Inter Milan 2009 akitokea Barcelona alipoisaidia kutwaa kombe la mabingwa chini ya Mourinho huko San Siro. Wakati huohuo ile ishu ya usajili wa mchezaji wa Argentina Angel Di Maria kwenda klabu ya Manchester United akitokea Real Madrid imemalizika rasmi usiku wa August 26 2014 baada ya Manchester United kuthibitisha kukamilisha usajili huo kwa ada ya uhamisho £59.7m. Ada hii ya uhamisho imeweka rekodi mpya ya uhamisho nchini Uingereza ikivunja rekodi ya Pauni milioni 50 ambayo Chelsea waliilipa Liverpool kwa ajili ya usajili wa Fernando Torres. Di Maria amekabidhiwa jezi namba 7 na amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia Manchester United.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako