• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Van Gaal asema hakushangazwa kufungwa na MK Dons

    (GMT+08:00) 2014-08-28 10:22:04

    Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amewaudhi wapenzi wa klabu hiyo baada ya kusema kuwa hakushangazwa na kichapo cha mabao 4-0 mikononi mwa klabu ya daraja la kwanza MK Dons katika mechi ya kuwania ubingwa wa kombe la Capital One. Man U ilibwagwa nje ya kombe hilo baada ya kushindwa katika mechi tatu za kwanza akiwa mkufunzi. Van Gaal alisema kuwa alikuwa anataka kujua uwezo wa kikosi chake cha pili haswa baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Sunderland wikiendi iliyopita. Van Gaal alitua Old Trafford baada ya United kumaliza katika nafasi ya 7 katika ligi kuu ya Uingereza na amewanunua wachezaji wengu tu kwa gharama ya pauni milioni 131.7 akiwemo mchezaji aliyegharimu kitita kikubwa zaidi katika ligi ya Uingereza Angel Di Maria aliyegharimu pauni milioni 59.7 alipotokea Real Madrid. Kichapo hicho kwa kikosi kilichogharimu chini ya nusu milioni kukiweka pamoja ni ishara ya jinsi hali imezidi kudorora tangu aondoke kocha Alex Fergusson.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako