• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kina Figo wapanda mlima Kilimanjaro

    (GMT+08:00) 2014-08-28 10:22:41

    Wakongwe wa klabu tajiri zaidi duniani Real Madrid ya Hispania ambao wako nchini Tanzania kwa ziara ya kitalii, juzi walipanda mlima Kilimanjaro na kujionea baadhi ya vivutio vya mlima huo mrefu zaidi barani Afrika. Nyota wakubwa wa soka wa zamani wa klabu hiyo wakiwamo wawili waliopata kushinda tuzo ya Ballon d'Or ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Luis Figo na Fabio Cannavaro, walikwenda Kilimanjaro. Baada ya kuwasili huko msafara wa wachezaji hao, ambao siku ya Jumamosi iliyopita walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya nyota wa zamani wa soka wa Tanzania na kuwafunga wenyeji wao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, walitua wakipokewa na mashabiki wengi. Timu hiyo yenye nyota kama Figo, Cannavaro, Christian Karembeu na mfungaji wa mabao matatu katika mechi dhidi ya wenyeji wao Tanzania, Ruben de la Red, walifika katika geti la Marangu majira ya saa 6:30 tayari kwa safari ya Kilomita 4 tu za kupanda na kujionea mandhari ya mlima huo wenye urefu wa mita 5,895.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako