• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN yataka walinzi amani waliotekwa nyara Golan waachie haraka

    (GMT+08:00) 2014-08-29 10:49:50

    Umoja wa Mataifa umetaka walinzi wa amani 43 wa umoja huo waliotekwa nyara na watu wenye silaha kwenye eneo linalotenganisha Israel na Syria kwenye milima ya Golan waachiwe huru bila masharti.

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw Stephane Dujaric amesema walinzi hao wa amani ambao wote wanatoka Fiji walitekwa nyara katika eneo la Quneitra, ambalo jeshi la Syria na wapinzani wamepambana vikali kugombea udhibiti wa kivuko pekee kati ya Syria na eneo la milima ya Golan linalodhibitiwa na Israel.

    Umoja wa Mataifa umesema bado haujathibitisha ni kundi gani lililowateka nyara watu hao, lakini msemaji wa umoja Bw Stephane Dujaric amesema kundi la Al Nusra limetangaza kuwajibika na utekaji huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako