• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rooney awa nahodha mpya wa Uingereza

    (GMT+08:00) 2014-08-29 11:13:31

    Mshambuliji wa Manchester United Wayne Rooney ametajwa kuwa nahodha mpya wa timu ya Uingereza na kocha Roy Hodgson. Mchezaji huyo amechukua nafasi hiyo kutoka kwa mchezaji wa Liverpool Steven Gerrard ambaye amestaafu baada ya Uingereza kutolewa kwenye michuano ya kombe la dunia. Rooney amefunga magoli 40 katika mechi 95, na mapema mwezi huu meneja wa United alimtaja kuwa nahodha wa klabu yake. Uingereza itacheza na Norway septemba 3 katika mchezo wa kirafiki kabla ya kampeni zao za kufuzu kucheza kombe la Ulaya mwaka 2016 kuanza. Wakati huohuo kipa wa zamani wa Arsenal Manuel Almunia ametangaza kustaafu baada ya kugunduliwa ana matatizo ya moyo yaliyonekana wakati anafanyiwa ukaguzi wa kawaida wa kiafya. Vipimo vimeonesha kuwa Alumunia ambaye amecheza mara 175 akiwa Arsenal anaweza kuwa na matatizo ya moyo ya kurithi ambayo yanaweza kupelekea kifo cha ghafla. Aluminia ameanza kibarua chake akiwa na klabu yake ya nyumbani nchini Hispania Osasuba mwaka 1999 kabla ya kujiunga na Arsenal mwaka 2004 akitokea Celta Vigo ambapo miaka minane baadaye alikwenda Watford.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako