• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michel Platini kutompinga Sepp Blatter kuwania urais wa FIFA mwakani.

    (GMT+08:00) 2014-08-29 11:14:54

    Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Uefa Michel Platini amesema hatompinga Sepp Blatter katika kura za kuwania urais wa FIFA mwakani.

    Rais huyo wa UEFA ambaye ni raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 59 awali alionesha nia ya kumpinga Blatter lakini jana aliwaambia wajumbe wa UEFA huko Monte Carlo kuwa anataka kuihudumua UEFA kikamilifu. Platini amewambia wajumbe hao 54 kuwa licha ya yeye kutaka Fifa isafishwe, anapendekeza kujitolea katika uongozi wa UEFA. Blatter mwenye miaka 78, ameongoza FIFA tangu mwaka 1998, lakini amekumbwa na upinzani mkali baada ya kuibuka tuhuma za hongo katika kinyang'anyiro cha kuwania uwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2022. Joto la kisiasa katika FIFA lilipanda majuzi baada ya Blatter kutangaza kuwania nafasi ya kuongoza FIFA kwa muhula wa tano. Kujiondoa kwake sasa kunamwacha Blatter akikabiliana na aliyekuwa katibu mkuu wa FIFA wa zamani Jerome Champagne. Wagombea wanapaswa kutangaza nia yao kuanzia Januari 2015, hata hivyo Platini atalazimika kusubiri hadi baada ya miaka mingine minne ili kuwania urais mwaka 2019. Platini, ameiongoza Uefa tangu mwaka 2007.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako