• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Samuel Eto'o na Xabi Alonso watangaza kustaafu soka ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2014-08-29 11:15:52

    Siku kadhaa baada ya Frank Lampard kutangaza kustaafu soka ya kimataifa, juzi ilikuwa siku nyingine kwa wanasoka wawili wa kimataifa nao kutangaza uamuzi wa kuachana na soka ya kimataifa. Samuel Eto'o na Xabi Alonso kwa nyakati tofauti juzi walitumia mitandao ya kijamii kutangaza uamuzi wao wa kuachana na soka ya kimataifa. Xabi Alonso kupitia mtandao wa Twitter kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Hispania. Kiungo huyo wa Real Madrid ameshaitumikia Hispania kwa muda wa miaka 11 na ameifungia nchi hiyo magoli 16 katika mechi 114.

    Wakati huo huo mfungaji mabao mengi zaidi wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto'o naye ametangaza kustaafu soka ya kimataifa.

    Mshambuliaji huyo ambaye ameifungia Cameroon mabao 56 amejiunga na Everton ya Uingereza juzi. Kufuatia kauli hiyo mshambuliaji huyo sasa hatakuwepo katika kipindi chote cha cha kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwezi Januari mwakani. Awali Cameroon ilifanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, kwa kuwaacha wachezaji 13 waliocheza kombe la dunia akiwemo Samuel Eto'o, kwa ajili ya mashindano yajayo ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako