• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji wadhibiti ubalozi wa Marekani nchini Libya

    (GMT+08:00) 2014-09-01 10:43:19

    Kundi moja la wapiganaji la Libya Fajr Libya limetangaza kudhibiti ubalozi wa Marekani mjini Tripoli, na "kulinda usalama" wa ubalozi huo, lakini Marekani bado haijaeleza lolote kuhusu habari hiyo.

    Tarehe 26 Julai Marekani ilifunga ubalozi wake nchini Libya na kuondoa wafanyakazi wake. Balozi wa Marekani nchini Libya Bibi Deborah Jones alisema, video iliyowekwa kwenye mtandao wa internet inayomuonesha mwanaume wa Libya akicheza kwenye bwawa la kuogelea la ubalozi huo, inaonekana kuwa ilipigwa katika eneo la makazi ya ubalozi huo, lakini hakuweza kuthibitisha.

    Habari zinasema kundi hilo halina uhusiano na kundi la Ansar al-Sharia linalotuhumiwa kumuua aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya Bw. Chris Stevens.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako