• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Homa ya hofu yapanda kati ya timu ya Liverpool na Real Madrid kwenye michuano ya Ulaya

    (GMT+08:00) 2014-09-01 10:45:31

    Liverpool inarudi katika michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu waliposhiriki mara ya mwisho mwaka 2009 na wamepangwa pamoja na Real Madrid ya Hispania, FC Basle ya Uswisi na Ludogorets ya Bulgaria. Wataikaribisha Real Madrid katika pambano la kwanza Oktoba 22 uwanjani Anfield kabla ya kusafiri kwenda katika mji mkuu wa Hispania, Madrid, Novemba 4 kwa ajili ya pambano la marudiano. Mara baada kutangazwa kwa ratiba hiyo, homa ilianza kupanda haraka baina ya timu hizo na Ronaldo amekiri kwamba kutakuwa na kasheshe kubwa atakaporudi Anfield ambako mara ya mwisho alicheza akiwa na timu pinzani ya Liverpool, Manchester United. Pambano hilo pia litarudisha nyuma kumbukumbu za ushindi wa mabao 4-0 wa Liverpool dhidi ya Real Madrid mwaka 2009. Lakini Ronaldo amewaonya mashabiki wa Liverpool kuwa matokeo hayo hayatajirudia. Achilia kundi hilo, Kundi A lina timu za Atletico Madrid, Juventus, Olympiakos na Malmo wakati kundi Kundi C kuna Benfica, Zenit St Petersburg, Bayer Leverkusen na Monaco. Katika Kundi D kuna timu za Arsenal, Borussia Dortmund, Galatasaray na Anderlecht wakati Kundi E lina timu za Bayern Munich, Manchester City, CSKA Moscow na AS Roma. Kundi F kuna Barcelona, PSG, Ajax na Apoel Nicosia wakati za Kundi G ni Chelsea, Schalke 04, Sporting Lisbon na Maribor huku Kundi H kukiwa na Porto, Shakhtar Donetsk, Athletic Bilbao na Bate Borisov.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako