• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fifa yakataa uchaguzi wa chama cha soka cha Nigeria

    (GMT+08:00) 2014-09-01 10:46:31

    Fifa imemkataa Chris Giwa ambaye amechaguliwa kuwa rais mpya wa Chama Cha Soka cha Nigeria NFF na kuonya kuwa nchi hiyo inaweza kufungiwa ikifika kesho jumanne kama hadi leo usiku atakuwa hajaachia madaraka. Hayo yote yamekuja kutokana na uchaguzi wenye utata wa NFF uliofanyika wiki iliyopita ambao ulisababisha mpasuko kwenye chama hicho. Fifa imesema haitambui kabisa uchaguzo huo, ingawa imesema inaonekana kwamba wizara ya michezo inautambua. Katika barua ya ijumaa Fifa ilikubali uamuzi wa wajumbe wengi wa baraza la NFF ambapo 39 kati ya 44 walilipigia kura baraza hili kuu, kwaajili ya uchaguzi wa kamati kuu ambao sasa utafanyika Septemba 4. Machafuko ndani ya NFF tayari yamepelekea Fifa iingilie kati, iipige marufuku Nigeria kushiriki kimataifa, hivyo marufuku nyingine inaweza kuiathiri Nigeria katika mechi ya kufuzu kucheza kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 dhidi ya Congo na Afrika Kusini mapema mwezi ujao. Juu ya yote hayo super eagles bado haina kocha wa kudumu baada ya mkataba wa Stephen Keshi kutoongezwa kufuataia kufanya vibaya kwenye kombe la dunia. Hata hivyo kocha huyo amekubali kukiongoza kikosi cha Nigeria kwa muda tu katika mechi mbili zijazo za kufuzu kucheza kombe la mataifa ya Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako