• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Je ni nini tunaweza kujifunza kutoka wa China kwenye kupambana na magonjwa ya maambukizi

    (GMT+08:00) 2014-09-07 17:51:00

    Bila shaka wasikilizaji mnaofuatilia habari kuhusu China, na habari za mambo ya Afya. Mtakuwa mnakumbuka kuwa China iliwahi kutikiswa na homa ya mafua makali ya SARS, na baadaye ilisumbuliwa na homa ya mafua ya ndege. Nakumbuka wakati ule hofu ilikuwa kama jinsi ilivyo sasa kwenye nchi za Afrika kuhusu Ebola. Je ni nini tunaweza kujifunza kutoka wa China kwenye kupambana na magonjwa ya maambukizi, kuwa nasi tukufahamishe.

    Pili: Kama tunavyojua kuwa China ni nchi kubwa na yenyewe watu wengi, kwa hiyo zikitokea dharura za kiafya kwa wakati fulani kunakuwa na mshikemshike. Kwa mfano karibu kila mwaka yanapokaribia majira ya baridi, huwa tunatahadharishwa kuwa makini na kujilinda dhidi ya mafua. Na hospitali huwa zinajiandaa vya kutosha kwa ajili ya watu wenye magonjwa yanayotokana na baridi na ya kuambukiza kama vile mafua au kikohozi, kwa hiyo wenzetu hata kwenye kalenda zao wanajua kabisa kuwa ikifika wakati fulani tunatakiwa kufanya nini ili tujilinde..

    Fadhili: Mbali na hayo wenzetu wako makini sana kupambana na magonjwa ya maambukizi kama vile mafua. Nakumbuka ulipotokea ugonjwa wa SARS na mafua ya ndege, kwa wataalamu wa afya walikuwa makini sana kutoa tahadhari kwa umma, na vyombo vya habari vilikuwa vinatoa habari vizuri kwa wananchi. Lakini uzuri ni kwamba hata wachina wenyewe ni wasikivu. Walipokuwa wanapewa maelekezo walikuwa wanasikia na kufuata kwa makini. Wakiambiwa wasitoke nje kama hawana jambo la muhimu walikuwa hawatoki.

    Pili: Kwa sasa nchi za Afrika na sehemu nyingine duniani zinakabiliwa na tatizo la homa ya Ebola. Ukiangalia jinsi nchi hizo zinavyopambana na Ebola na changamoto zake, unaweza kuona kuna mengi ya kuiga na kujifunza kutoka kwa China na kuwa na manufaa kwenye vita dhidi ya Ebola. Siku chache zilizopita nakumbuka kulikuwa na video zimewekwa kwenye mtandao wa youtube zikionesha baadhi ya watu katika nchi zilizoathiriwa na Ebola wakipuuza maelekezo ya wataalamu wa afya. Hali kama hii hapa China si rahisi kutokea, wananchi ni wasikivu.

    Fadhili: Nakumbuka wakati a Ugonjwa wa SARS wataalam wa afya walisema chanzo kilikuwa ni nyama pori, na wakapiga marufuku nyama hiyo kuliwa. Lakini baadhi ya watu tuliowaona kwenye mtandao wa youtube walipokatazwa kula nyama wao walikuwa wanabisha.

    Pili: Kuna mengine naweza kusema hata ni ya aibu, kwa mfano serikali ya Liberia ilianzisha kituo cha karantini, baadhi ya waporaji walivamia kituo hicho na kupora vitu, watu waliokuwa wamewekwa kwenye karantini walikimbia, sasa uzembe na ukaidi kama huu unatokana na kupuuza onyo kutoka kwa wataalamu wa afya. Kwa wenzetu wachina vitu kama hivi si rahisi kutokea.

    Fadhili: Nakumbuka moja kati ya mambo yaliyokuwa yanaagizwa na serikali ni kuwa wauza nyama, kwa mfano wanaouza kuku na bata, wakati wa ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege karibu wote waliacha kuuza nyama hiyo. Hata mayai yalikuwa hayauzwi, na sehemu nyingine watu waliagizwa kuchinja kuku na bata, karibu kuku na bata wote walichinjwa.

    Pili: Umezungumzia karantini hii ni njia yenye ufanisi kuzuia magonjwa ya maambukizi. Lakini kwa wale wanaolazimika kusafiri kwanza huwa wanakaguliwa kuhakikisha kuwa hawasafirishi ugonjwa. Mfano mmoja ambao unasikitisha, ni ule wa raia wa Liberia aliyekwenda Nigeria. Kwanza aliambiwa asisafiri, lakini yeye alisafiri, lakini swali lingine ni kuwa aliruhusiwa kuingia kwenye ndege bila kupimwa. Hapa wenzetu China kwenye viwanja vya ndege wanaweka vifaa kupima joto la abiria bila mwenyewe kujua, ili kujua ni abiria gani anaweza kuwa mgonjwa.

    Fadhili: Jambo lingine ambalo naweza kusema linasikitisha ni kuona jinsi utoaji wa habari kuhusu ugonjwa wa Ebola zilivyo holela. Kwa hapa China ni nadra sana kusikia watu wanatoa habari ovyo, hasa kuhusiana na hatari kama magonjwa ya mlipuko. Kwa mfano tumesikia mara kadhaa watu wanasema Ebola imeingia Kenya, lakini baadaye serikali inakanusha, tumesikia baadhi ya vyombo vya habari vinasema wagonjwa wawili wa Ebola wamegunduliwa Tanzania lakini baadaye serikali ikakanusha, kwa hiyo tunaona kabisa kuwa kuna tatizo la utoaji holela wa habari.

    Pili: Vilevile kuna baadhi ya waandishi wa habari ambao licha ya kutoa habari za kweli, upande wa habari wanazotoa unakuwa na utata. Kwa mfano mwandishi moja wa habari wa Guinea, alikuwa anahimiza dawa ya majaribio ya Zmapp itolewe kwa wagonjwa wengi zaidi wa Afrika magharibi, lakini hakuhimiza hata kidogo watu wachukue tahadhari za msingi za kiafya ili kuepuka ugonjwa huo. Kidogo hii naweza kusema ni sawa na kuwataka watu wasubiri moto uwake ndio wahangaike kuuzima, badala ya kuwahimiza wachukue hatua za kuzuia kutokea kwa moto. Njia ya namna hii kwenye mazingira ya nchi kama Tanzania kwa kiasi fulani haifai, wakati mwingine hata kama dawa yenyewe ikipatikana huenda hata waliambukizwa watashindwa kumudu kununua.

    Fadhili: Jambo moja ambalo tumeliona hapa China, ni kuwa wenzetu kwanza huwa wanaandika na kutangaza zaidi habari kuhusu ugonjwa wenyewe, namna unavyoambukizwa na kuenea, na namna ya kujikinga. Suala la dawa na namna ugonjwa huo unavyotibiwa, hili ni la kuwaachia madaktari na wataalamu wengine wa afya, na sio waandishi wa habari. Labda waandishi wa habari waandike kile wanachoambiwa na madaktari na wataalamu wa afya.

    Pili: Kwa upande mwingine naweza kusema hapa ni maswala ya usimamizi wa vyombo vya habari, hasa kwenye kutangaza habari zinazohusiana na mambo ya dharura, kama tulivyodokeza mwanzo, wenzetu hawatangazi habari hizo ovyo, kunakuwa na utaratibu maalum sio kila mtu anaweza kutoa maoni kutokana na uelewa mdogo kuhusu jambo lenyewe.

    Fadhili: Vile vile kumekuwa na kitu kama uelewa usio sahihi kuhusiana na magonjwa haya ya maambukizi, kuna wengine wanaona kuwa ukiwa maskini basi wewe unakuwa na hatari ya kuambukizwa, na ukiwa tajiri basi huna hatari. Hali halisi sio hivyo, mfano mzuri ni China, hii ni nchi tajiri lakini tumeona kuwa ilisumbuliwa sana na SARS na mafua ya ndege. Kikubwa wanachofanya wenzetu ni kuhakikisha kuwa elimu ya kupambana na magonjwa inapewa kipaumbele, sambamba na tiba.

    Pili: Hata kwenye nchi zetu nadhani tatizo lililopo ni kupuuza. Siku zote tunaambiwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba, kwa hiyo kama tukiwa makini kwenye kuhakikisha kuwa hatuambukizwi magonjwa kama mafua au Ebola na hatuingii kwenye mazingira ya kuwaambukiza wengine, basi tunaweza kuwa salama, hata kama si matajiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako