• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gazeti la CPC lapongeza uamuzi uliopitishwa na bunge la umma la China kuhusu mageuzi ya uchaguzi wa Hong Kong

    (GMT+08:00) 2014-09-01 19:17:49

    Gezeti la chama cha kikomunisti cha China People's Daily, limepongeza uamuzi uliopitishwa na bunge la umma la China kuhusu mageuzi ya uchaguzi wa eneo la utawala maalum la China, Hong Kong, likisema uamuzi huo ni hatua muhimu kwa ajili ya maendeleo ya mfumo wa kisiasa wa eneo hilo.

    Uamuzi huo unaweka bayana kuwa kuanzia mwaka 2017, mmoja kati ya wagombea wawili au watatu atachaguliwa moja kwa moja kuwa mkuu wa Hong Kong kwa kupitia kura zitakazopigwa na watu wa Hong Kong. Wagombea hao watachaguliwa kabla ya hapo na kamati yenye uwakilishi mpana.

    Tahariri iliyotolewa na gazeti hilo inasema, kutekelezwa kwa uchaguzi wa moja kwa moja wa mkuu wa Hong Kong kuna umuhimu mkubwa kwa sera ya Nchi Moja, Mifumo Miwili, na mamlaka na usalama wa taifa la China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako