• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mourinho na Terry wasuuzwa na uchzaji wa Diego Costa

    (GMT+08:00) 2014-09-02 10:40:43

    Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amekiri kwamba Diego Costa staa aliyemnunua kutoka Atletico Madrid kwa dau la Pauni milioni 32 ni ni moto wa kuotea mbali na ni shida kwa mabeki. Costa alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 6-3 wa Chelsea dhidi ya Everton juzi usiku na kuifanya Chelsea iendelee kukamata kilele cha Ligi Kuu ya England ikiwa na pointi tisa. Mourinho alisema Diego alipata nafasi tatu na kufunga mabao mawili. Nafasi nyingine ilikuwa ni juhudi kubwa ya Tim Howard kuokoa, kwa hiyo ni mmaliziaji mzuri, lakini amesisitiza kuwa hachangii hilo tu, kwani pia anashiriki katika kila kitu hadi ulinzi. Kama vile haitoshi, Costa alisifiwa vilivyo na nahodha wake, John Terry pamoja na mchambuzi wa soka, Jamie Redknapp ambaye ni nyota wa zamani wa Liverpool na Timu ya Taifa ya England. Hata hivyo, licha ya kupongezwa huko, nyota huyo wa Hispania mzaliwa wa Brazil alilaumiwa vikali na Kocha wa Everton, Roberto Martinez kwa kile kinachodaiwa kuwa alimkejeli mlinzi wa Everton, Seamus Coleman baada ya kujifunga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako