Michuano ya kombe la Afrika maarufu kama Africa Cup of Nations inayotarajiwa kutimua vumbi nchini Sierra Leone, ambayo itachuana na Ivory Coast itaendelea kama ilivyopangwa japokuwa kuna tishio la ugonjwa wa Ebola. Shirikisho la mpira wa Miguu nchini Sierra Leone limejinasibu kutaja kikosi chake kitakacho menyana na Ivory coast na kuelezea kuwa orodha hiyo itakua imejaa wachezaji kutoka ng'ambo. Ivory coast imetahadharisha kwa kusema kwamba michuano hiyo haitapangwa kufanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Abidjan, kwa kuhofia maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola. Japokuwa haijatangwazwa eneo mbadala na hatari inayotishia michuano hiyo. Huko Nigeria, mjane wa daktari wa sita kukumbwa na ugonjwa wa Ebola naye ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo. Taarifa nyingine zinaeleza kwamba madaktari watatu wamepelekwa katika kituo cha utafiti na ufuatiliaji ugonjwa wa Ebola, japokuwa hawajathibitika kuambukizwa ugonjwa huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |