Kocha wa Uganda Milutin 'Micho' Sredojevic juzi alisema anategemea kupata matokeo mazuri kwenye mechi ya kufuzu kombe la Afcon mwaka 2015 dhidi ya Ghana. Timu hiyo iliondoka Uganda na kuweka kambi yake Niamey Niger kabla ya kuelekea Kumasi, Ghana kucheza mechi ya kundi E septemba 5. Uganda pia leo inakwaana na Niger huko Niamey katika mechi ya kirafiki ambapo timu hizo mbili zitaitumia kujiandaa kwa michuano ya kufuzu kombe la Afcon. Katika mechi hizo Niger itapambana na Cape Verde. Hata hivyo timu ya Sredojevic ilisafiri ikiwa na wachezaji 14 tu, wakati watano wa kimataifa wataungana nao huko Niger. Mshambuliaji Brian Umony amesema ingawa Ghana ni timu kubwa katika soka ya Afrika, watajitahidi kuhakikisha wanapata ushindi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |