• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Nigeria laweka marufuku ya kutoka nje usiku katika ngome ya kundi la Boko Haram

    (GMT+08:00) 2014-09-02 11:03:06

    Jeshi la Nigeria limetekeleza marufuku ya kutoka nje usiku huko Maiduguri, ambako ni ngome ya kundi la Boko Haram katika kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno.

    Msemaji wa divisheni ya 7 ya jeshi la Nigeria Kanali Sani Usman amesema marufuku hiyo inatekelezwa kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi, lakini hakutaja muda wa kutekeleza marufuku hiyo. Amesema huenda marufuku hiyo itaendelea kutekelezwa hadi jeshi la Nigeria litakapoona jimbo la Borno "lina usalama wa kutosha". Pia ametoa mwito kwa wakazi wa huko washikamane ili kupambana na magaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako