• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usajili wa wachezaji kimataifa wafikia ukingoni

    (GMT+08:00) 2014-09-03 11:19:34

    Dirisha la kimataifa la usajili limefungwa juzi huku Manchester united wakiibuka kidedea. Man United imevipiku vilabu vingine vya soka baada ya kumnyakua mshambuliaji nguli Radamel Falcao kutoka klabu ya Monaco kwa kiasi cha pound milioni 6, huo ukiwa ni mkopo wa muda mrefu. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akiwa na klabu ya Monaco hadi anafungasha virago na kuondoka ameifungia Monaco ya Ufaransa jumla ya mabao 11 katika mechi 20. Nao Arsenal wamemchukua mshambuliaji wa Man United Danny Welbeck kwa mkopo wa pound million 16. Matumaini ni makubwa kwa mshambuliaji huyo anayetua katika uwanja wa Emirates huku mashabiki wake wakionyesha Imani kubwa kwake katika msimu huu. Wakati huohuo Southampton imemsajili mchezaji wa Senegal Sadio Mane kutoka katika klabu ya Austria ya Red Bull Salzburg kwa pauni milioni kumi. Kwa mujibu wa meneja Ronald Koeman, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye ameingiza mabao 45 katika mechi 87, wakati wa msimu wa ligi ya nchi hiyo, anaweza kucheza kama kiungo cha kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako