• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirikisho la soka la Nigeria kuishtaki Schalke kwa kutomruhusu Obasi

    (GMT+08:00) 2014-09-03 11:20:07

    Shirikisho la soka nchini Nigeria limesema litaishitaki klabu ya Schalke ya Ujerumani kwa Fifa baada ya klabu hiyo kukataa kumruhusu mshambuliaji Chinedu Obasi kushirki michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015. Hata hivyo klabu ya Schalke imesema sababu ya kutomruhusu mchezaji huyo kuondoka ni kwamba pasi yake ya kusafiria iko katika ubalozini akitayarishwia viza yake kabla ya kuanza kwa michunao ya klabu bingwa Ulaya. Afisa wa habari wa Super Eagles Ben Alaiya amesema wana mechi mbili ambazo tayari zimeidhinishwa na Fifa. Nigeria ambao ni mabingwa wa Afrika, watamenyana na Congo tarehe sita Septemba. Siku nne baadaye watatoana kijasho na Afrika Kusini. Nigeria imekasirishwa na Schalke kuhusu mchezaji wake Obasi. Vilabu hushurutishwa kuwaruhusu wachezaji wa kigeni kuchezea nchi zao katika michunao ya kimataifa pindi wanapotakiwa na nchi zao kucheza. Klabu hiyo ya Bundesliga inamtaka Obasi, kucheza dhidi ya Borussia Monchengladbach katika ligi hiyo na mechi itakayochezwa dhidi ya Chelsea katika michuano ya klabu bingwa Ulaya tarehe 13 na 17.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako