• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya wamkumbuka Waldegard kwa hisia kubwa

    (GMT+08:00) 2014-09-03 11:21:33

    Kenya itaendelea kumkumbuka Bjorn Waldegard kwa hisia kubwa, mswiden ambaye ni dereva wa mashindano ya magari ambaye mwaka 1979 alikuwa dereva wa kwanza kushinda mbio ndefu za magari za world Rally Championship WRC. Waldegard aliyefariki dunia Agosti 30, alishinda mbio za Safari Rally, ameelezwa kuwa ni dereva imara, wa muda mrefu na mwenye changamoto nyingi katika mfululizo wa mashindano ya WRC ya mwaka 1977, 1984 na mwaka 1990. Dereva wa zamani wa mbio hizo za magari za nyika Phineas Kimathi amesema sifa kubwa ya Waldegard ni kwamba alikuwa ngangari katika mashindano hayo katika njia zenye matope na kavu katika ardhi ya Afrika, na kueleza kuwa ushindi unategemea zaidi mbinu za dereva, kitu ambacho alikuwa nacho. Kwa miaka 30 mashindano ya magari ya Safari Rally yamekuwa yakifanyika kwa siku nne katika kipindi cha sikukuu ya pasaka, ambapo Waldegard na wenzake wameufanya ulimwengu mzima kuganda kwenye redio na televisheni zao wakiangalia na kusikiliza mashindano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako