• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya jezi 5,000 zenye namba ya Kagawa zauzwa kwa masaa kadhaa

    (GMT+08:00) 2014-09-04 10:51:39

    Dirisha la usajili barani ulaya limefungwa juzi usiku, Shinji Kagawa ni mmoja wa wachezaji waliofanya uhamisho katika dirisha hili la usajili. Kiungo wa Japan, aliuzwa kutoka Manchester United kwenda Borussia Dortmund kwa ada ya uhamisho wa £ 6.3 million. Fedha hizo walizolipa Dortmund zinaweza kuwa zimerudi ndani ya siku kadhaa baada ya ripoti ya gazeti la BILD kusema kwamba mauzo ya jezi namba 7 atakayoivaa Kagawa akiwa Dortmund yamekuwa ya kasi mno. Ripoti zinasema jezi ya Shinji Kagawa iliuzwa mpaka kufikia idadi ya jezi 5,000 katika kipindi cha masaa kadhaa tangu alipotangazwa rasmi kurudi kwenye klabu yake hiyo aliyohama na kwenda United mnamo mwaka 2010. wakati huohuo Miezi miwili baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia, huku timu ya taifa ya Ujerumani ikitwaa ubingwa wa dunia, nahodha wa timu hiyo Philip Lahm alifikia uamuzi wa kujiuzulu kuichezea timu hiyo na hivyo kuacha wazi nafasi ya unahodha kwenye timu hiyo, baada ya Lahm kujiuzulu, kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low amemteua nahodha mpya wa timu hiyo.Kiungo wa FC Bayern Munich Bastian Schweinsteiger ndio amerithi nafasi iliyoachwa wazi na Philip Lahm. Bastian mwenye miaka 30 ameshaichezea Ujerumani kwenye mechi zaidi ya 100 tangu alipoanza rasmi kuitumikia timu hiyo mwaka 2004. Manuel Neur pia ameteuliwa kuwa nahodha msaidizi wa Ujerumani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako