Klabu kubwa ya Kenya Gor Mahia imemuajiri kocha mpya kutoka Scotland Frank Natal kumrithi kocha aliyepita Bobby Williamson na kufanyakazi kama kocha mkuu ambapo sasa atatumikia kipindi cha uangalizi kwa miezi mitatu. Williamson ambaye aliacha kazi hivi majuzi kwenye timu hiyo ili aweze kuiongoza timu ya taifa, alichagua mrithi wake huyo ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Glascow Celtic kuchukuwa utawala wa timu hiyo ambayo ameiongoza na kuwa mabingwa wa msimu uliopita, kwenye ligi kuu ya Kenya kwa mara kwanza katika miaka 18. kocha huyo mpya aliwasili Kenya juzi jumatano asubuhi na kukaribishwa rasmi siku hiyo mchana kwa maandalizi ya mechi yake ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Simba Sports Club ya Tanzania, itakayochezwa kesho jumamosi. Kocha wa muda Frank Ouna amekuwa kocha msaidizi pamoja akishirikiana na kocha msaidizi wa sasa Bobby Ogolla.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |