• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Welbeck ang'ara katika ushindi wa Uingereza dhidi ya Uswisi

    (GMT+08:00) 2014-09-10 14:03:16

    Uingereza imeanza vizuri kampeni zake za kusaka tiketi ya kucheza fainali za kombe la Ulaya zitakazofanyika huko nchini Ufaransa mwaka 2016, wakati mshambuliaji aliyesainiwa na Arsenal hivi majuzi kwa ada ya pauni milioni 16 Danny Welbeck akiipatia ushindi timu yake wa mabao 2-0 dhidi ya Uswisi. Upande wa meneja Roy Hodgson ulihitaji kuonesha mchezo mzuri na kuleta matokeo bora baada ya balaa lililowakumba nchini Brazil kwenye michuano ya kombe la dunia kwa kutolewa katika hatua ya makundi. Uswisi ambao wako nafasi ya 9 katika viwango viliyotajwa na FIFA mwezi Agosti baada ya kufika katika raundi ya timu 16 katika kombe la dunia, huku Uingereza ikiwa nafasi ya 20, ilikuwa ni tishio kubwa kwa Uingereza lakini iliishia kukandamizwa kisawasawa magoli mawili bila jibu. Welbeck alifunga magoli hayo katika dakika ya 58 na 90.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako