• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wenger achanganyikiwa hajui ampange nani kwenye kikosi chake

    (GMT+08:00) 2014-09-10 14:03:43

    Kibarua kikubwa kinamkabili Arsene Wenger msimu huu klabuni Arsenal, baada ya kutojua ampange nani na amwache nani kwenye kikosi chake hasa kwa mastaa wake, Santi Cazorla na Mesut Ozil. Msimu uliopita wimbi la majeruhi lilimtibua kwani alibakiwa na wachezaji wachache tu waliokuwa fiti kucheza jambo ambalo halikuumiza kichwa kwenye uteuzi wa kikosi ambapo Cazorla na Ozil walianzishwa pamoja. Alexis Sanchez, Danny Welbeck na Joel Campbell wameongezeka kwenye safu hiyo. Alex Oxlade-Chamberlain, Lukas Podolski na Theo Walcott waliokuwa majeruhi kwa muda mrefu msimu uliopita wamerudi na kuongeza idadi kwenye safu hiyo. Wenger anahaha kutafuta nafasi ya kuchezesha viungo wake Ozil na Cazorla, tatizo lililopo kwa sasa hawawezi kucheza wote kwa pamoja, tatizo ni nani aanzie benchi? Msimu uliopita walicheza wote kwa pamoja, Cazorla kushoto na Ozil katikati. Msimu huu Ozil amepangwa kushoto, lakini Walcott atakaporudi itakuwa tatizo. Upande huo huo wa kushoto kutakuwa na Sanchez kama Welbeck ataanza vizuri kama straika. Kuna Podolski, Campbell, Oxlade-Chamberlain, Yaya Sanogo na Olivier Giroud akirudi uwanjani itakuwa balaa zaidi. Hiyo ina maana Wenger atalazimika kuwashusha Cazorla na Ozil kwenye kiungo mahali ambapo tayari kuna watu makini, Aaron Ramsey, Mikel Arteta na Jack Wilshere. Kutokana na hilo, Cazorla na Ozil watagombea nafasi moja tu, kucheza Namba 10 na hivyo mmoja lazima aanzie benchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako