Marin Cilic wa Croatia ameibuka bingwa wa US Open kwa kumfunga Kei Nishikori wa Japan. Mpambano huo umechezwa katika uwanja wa Arthur Ashe Mjini New York Marekani. Cilic amepokea kombe la michuano ya tennis upande wa wanaume kwa mara ya kwanza baada ya kumshindilia mpinzani wake seti tatu za 6-3, 6-3, 6-3. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya fainali za US Open ambapo mechi ya fainali inawakosa mmoja kati ya wachezaji wakali akiwemo Andy Murray, Novak Djokovic ama Roger Federer. Cilic anakuwa Mkroatia wa kwanza kutwaa ubingwa wa moja kati ya mashindano makubwa manne ya tenis duniani tangu kocha wake Goran Ivanisevic abebe ubingwa wa Wimbledon mwaka 2001. Wakati huohuo bingwa huyo amesema ushindi wake utawavutia wachezaji wengine wa tenisi na kuwafanya wawe wachezaji bingwa wa mchezo huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |