Manchester United imeripoti kuwa mapato yake yamepanda kwa asilimia 19 ambazo ni sawa na pauni milioni 433.2, lakini faida imepungua kwa asilimia 84. Klabu hiyo ya Uingereza, imekadiria kuwa mapato na faida vitashuka mwaka 2015 kutokana na kuzidi kupata matokeo mabaya, hasa katika mashindano ya ligi kuu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20. Makadirio hayo yanakuja huku ikiripotiwa kuporomoka kwa kasi faida, licha ya rikodi za mapato za mwaka 2014. Aidha, matokeo hayo pia yanaonesha kuwa Moyes na wafanyakazi wake walipata jumla ya Dola milioni nane za kimarekani kama malipo ya kuachishwa kazi mapema mwaka huu baada ya kuwa ofisini kwa chini ya mwaka mmoja. Wakati huohuo makamu mwenyekiti mtendaji wa clabu hiyo Ed Woodward amesema United ipo ukingoni kupata kitu maalumu licha ya kwamba ripoti za kushuka kwa faida. Amesema msimu wa 2013/14 ulikuwa na changamoto nyingi na kukaatisha tama, lakini wanafurahia kwa kuwa na meneja bora duniani ambaye anaweza kugeuza mambo. Woodward amesema atalenga zaidi katika kupandisha kodi ya mapato pamoja mapato ya matangazo ambayo yameongezeka kwa asilimia 24 kufuatia adidas kuthibitisha kuwa wamekubali kutengengeza fulana mpya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |