Rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa), Michel Platini, amemchimbia mkwara Franck Ribery kwa kumweleza kwamba atamfungia kucheza mechi tatu za soka kama atagoma kurudi kwenye kikosi cha Ufaransa. Staa huyo wa Bayern Munich alitangaza kustaafu soka ya kimataifa, lakini Platini alisema uamuzi wa kufanya hivyo si wa mchezaji bali ni wa kocha wa timu ya taifa ambaye ndiye mwenye majukumu ya kutaja wachezaji. Ribery alikosa fainali za Kombe la Dunia 2014 zilizofanyika nchini Brazil kutokana na kuwa na majeraha na baadaye Agosti aliamua kutangaza kustaafu soka ya kimataifa. Platini alisema uamuzi wa Ribery wa kustaafu hautakuwa sahihi hadi kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps aamue kwamba kweli mchezaji huyo anastahili kuondolewa kwenye kikosi. Platini alisema huo si uamuzi wa wachezaji kama wanataka au hawataki kuichezea timu ya taifa bali ni uamuzi wa kocha. Na kusisitiza kuwa kama kocha amemtaka Franck Ribery akacheze, basi lazima aende na endapo akigoma atamfungia mechi tatu za Bayern Munich. Zaidi ya hayo amesema hatatamwelewa kabisa kwasababu yeye ni Mfaransa na michuano ya ubingwa wa Ulaya 2016 itafanyika Ufaransa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |