• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Klabu moja ya Ulaya 'yaendeshwa na wahalifu', asema mkuu wa zamani wa ligi

    (GMT+08:00) 2014-09-11 14:17:21

    Mkuu wa zamani wa ligi ya soka ya kulipwa ya Ulaya Emanuel Medeiros amedai kuwa klabu moja kubwa ya Ulaya inaendeshwa na wahalifu. Medeiros anaamini kuwa klabu hiyo, ambayo hakuitaja jina, inaendeshwa na mtandao wa upangaji wa uhalifu kupitia kampuni yao. Amesema ana ushahidi, lakini hawezi kuitaja klabu hiyo na ipo kwenye nchi gani. Medeiros ambaye kwa sasa ni mkuu wa kituo cha kimataifa cha usalama wa michezo ICSS, amesema hili sio jambo geni, wamekuwa wakifahamu masuala haya tangu mwaka 2003, lakini uchunguzi wa polisi bado unaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako