• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pistorius asafishwa kuwa kaua bila kukusudia

    (GMT+08:00) 2014-09-12 14:53:18

    Jaji anayetoa uamuzi katika kesi inayomkabili Oscar Pistorius, Thokozile Masipa jana alitoa hukumu juu ya mashtaka ya mauaji yanayomkabili mwanariadha huyo kwamba ameuua bila kukusudia, lakini ameacha hadi leo kutangaza kama Pistorius anastahili adhabu kwa mauaji hayo. Jaji huyo amesema upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitishia kikamilifu kwamba Pistorius alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa makusudi chooni. Hata hivyo alisema Pistorius alichukua hatua haraka na kitendo chake hicho ni wazi kilikuwa cha uzembe. Akiahirisha kesi hiyo hadi leo jaji Masipa alisema mtu mwenye busara asingefyatua risasi. Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana lakini amekana kumuua kwa maksudi, akisema alidhani mwizi alikuwa amevamia nyumba yake. Pistorius amekanusha mashtaka yote yanayomkabili, yakiwemomawili ya kufyatua risasi hadharani na kumiliki silaha kinyume cha sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako